Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na wawakilishi wa jumuiya za kiraia DR Congo

Ban akutana na wawakilishi wa jumuiya za kiraia DR Congo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na mkutano hii leo na wawakilishi wa walio wengi, wanasiasa wa upinzani na jumuiya za kiraia mjini Kinshasa.

Katika mkutano nao amesisitiza umuhimu wa majadiliano ya kisiasa kama njia ya kushughulikia changamato zinazohusiana na mchakato wa uchaguzi. Wamewataka viongozi wa kisiasa kuonyesha busara na kushiriki kikamilifu majadiliano ambayo anatumai yatasaidia kuwa na uchaguzi wa amani na wa uhakika kwa wakati ukizingatia katiba.

Katibu mkuu amezipongeza jumuiya za kiraia kwa kuchagiza mijadala ya kidemokrasia na kuchangia kutafuta suluhu muafaka ya mkwamo wa sasa wa kisiasa.

Kabla ya hapo Ban alikutana na waziri mkuu wa nchi hiyo Matata Ponyo Mapon, na kisha waziri wa mambo ya nje bwana Raymond Tshibanda,ambapo walijadili siasa na hali ya usalama nchini DR Congo na eneo zima la maziwa makuu.