Skip to main content

IAEA yasaidia Brazil kuimarisha mapambano dhidi ya mbu wanaobeba virusi vya Zika

IAEA yasaidia Brazil kuimarisha mapambano dhidi ya mbu wanaobeba virusi vya Zika

Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, IAEA litapeleka bomba la kununurisha mionzi ya gamma nchini Brazil, ili lisaidie nchi hiyo katika mapambano dhidi ya mbu wanaobeba virusi vya Zika. Taarifa kamili na Flora Nducha

(TAAIFA YA FLORA)

Shirika hilo limetangaza hayo katika mkutano wa siku mbili wa wataalam kutoka nchi 12, ambao umefanyika katika mji mkuu wa Brazil, Brasilia.

Bomba hilo linalonunurisha mionzi inayowafanya wadudu dume kuwa tasa, linaweza kusaidia kuongeza kasi ya kuzalisha mbu dume walio tasa katika miezi michache, na kisha wakasambazwa katika maeneo ya nchi hiyo yaliyoathiriwa na mlipuko wa sasa wa virusi vya Zika.

Taarifa ya IAEA imesema  kuwa mbu dume walio tasa wakijamiiana na mbu wa kike, wanakuwa hawawezi tena kuzalishana na kwa njia hii, idadi ya mbu wanaobeba virusi vya Zika watapungua kwa kiwango kikubwa katika siku zijazo.