Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa ndani wamtaka Ban kushinikiza serikali ya mseto Sudan Kusini

Wakimbizi wa ndani wamtaka Ban kushinikiza serikali ya mseto Sudan Kusini

Wakimbizi wa ndani Sudan Kusini ambao wanapata hifadhi kwenye majengo ya Umoja wa mataifa mjini Bentiu wametoa wito kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kutia shinikizo kwa pande kinzani nchini humo kwa mkataba wa amani wa mwezi Agosti ili kuunda serikali ya umoja wa kitaifa haraka iwezekanavyo ili kukomesha madhila kwa mamilioni ya raia.

Radio Miraya ambayo ni ya Umoja wa Mataifa nchini humo imezungumza na baadhi ya wakimbizi wa ndani kwenye kambi ya Bentiu kuhusu matarajio yao katika ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inayotarajiwa, na haya ndio waliyosema..

(SAUTI YA IDP’S)

“Bila shaka kama raia tumechoshwa na kinachoendelea na tunatarajia ziara yake kutoa shinikizo kwa pande mbili kinzani ili wahakikishe kwamba muafaka wa amani wa mwezi Agosti unatekelezwa kama ulivyosainiwa. Hivyo tunamtarajia kuzishinikiza pande hizo ili ziunde serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa mara moja. Ntapenda azungumzie amani Sudan Kusini pia ntapenda achagize amani Sudan Kusini pamoja nasi”.

Ban Ki-moon anatarajiwa kuwasili Sudan Kusini kesho Alhamisi.