Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sekta binafsi chocheeni mabadiliko chanya Maziwa makuu- Ban

Sekta binafsi chocheeni mabadiliko chanya Maziwa makuu- Ban

Akiwa kwenye ziara yake ya kusaka kuboresha masuala ya kiutu huko Ukanda wa Maziwa Makuu, Afrika, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumza kwenye mkutano wa uwekezaji wa sekta binafsi huko Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na kusihi viongozi wa ukanda huo, sekta binafsi na wadau wa maendeleo kusaidia kuondoa vichochezi vya mizozo na migongano. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Assumpta)

Ban amesema mizozo inayoendelea kwenye ukanda huo imezuia wakazi wake kustawi licha ya rasilimali lukuki zilizosheheni akisema ni vyema kuchukua hatua siyo tu kutatua mizozo bali pia kushughulikia vyanzo vyake ili kuweka mazingira bora ya ustawi.

Amesema mkutano huo ni mwendelezo wa utekelezaji wa mkataba wa amani, ulinzi na usalama kwa maziwa makuu uliotiwa saini miaka mitatu iliyopita , akisisitza kuwa unaweka mazingira ya kufanikisha ajenda ya maendeleo endelevu hivyo akasema..

(Sauti ya Ban)

Kwa hili, ni vyema kuweka msingi mzuri na tulivu wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. inahitaji utawala bora na utawala wa kisheria. Tunahitaji jamii yenye afya, iliyoelimika na yenye ari. Fursa hii lazima ipatiwe wanawake na wanaume wote na waweze  kuwa na ajira zenye staha.”

Kwa upande wake Rais Joseph Kabila amesema sasa wako katika kutekeleza miradi kipaumbele 25 ya ujumuishi ikiwemo miundombinu, kilimo, sekta ya nishati na utalii na hivyo..

(Sauti ya Kabila)

"Inabidi tuendelee na juhudi zetu ili kuondoa vikwazo vyote dhidi ya  safari huru za watu, bidhaa na fedha kwenye ukanda huo.”