Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN Women inasaidia taasisi ya uongozi wa kitaifa Sudan Kusini:

UN Women inasaidia taasisi ya uongozi wa kitaifa Sudan Kusini:

Taasisi ya uongozi maalumu kwa ajili ya kudhibiti migogoro , kuchagiza Amani na kuwezesha wanawake kiuchumi imefunguliwa mjini Juba Sudan Kusini.

Taasisi hiyo ya kitaifa ya kuleta mabadiliko inatoa programu zinazojikita katika mafunzo na uelimishaji kuhusu mabadiliko ya uongozi na maendeleo endelevu.

Wataalamu 17 wamepatikana kutoa mafunzo. Taasisi hiyo imeanzishwa na wizara ya jinsia, watoto na ustawi wa jamii kwa msaada mkubwa wa kitengo ya Umoja wa mataifa kinachohusika na masuala ya wanawake UN Women.

Akizungumza katika uzinduzi wa taasisi hiyo mkurugenzi wa mipango wa UN Women anayezuru Sudan Kusini ,Maria Noel Vaeza amesisitiza umuhimu wa kuwawezesha wanawake nchini humo.