Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasaidia kurejesha kwa hiyari waathirika wa usafirishaji haramu wa watu kutoka Nigeria, Sierra Leone

IOM yasaidia kurejesha kwa hiyari waathirika wa usafirishaji haramu wa watu kutoka Nigeria, Sierra Leone

Kwa ushirikiano na serikali ya Kuwait Shirika la Kimataifa la Uhamiaji(IOM) linatoa usaidizi wa kurejea nyumbani kwa hiyari na kuwajumuisha katika jamii waathirika wa usafirishaji haramu wa watu kutoka nchini Nigeria na Sierra Leone.

Wanawake wawili wamekuwa wakiishi kwenye malazi ya serikali ya Kuwait kwa ajili ya wafanyakazi wa kigeni kwa miezi mitano na ni watu wa kwanza waathirika wa usafirishaji haramu kusaidiwa na IOM nchini humo.

Serikali ya Kuwait imetambua umuhimu wa kuwasaidia watu hao kurejea nyumbani na kujumuishwa katika jamii na sasa inafanya majadiliano na ofisi zake za ndani husika ili kuimarisha utaratibu huo.

Mwaka 2015 serikali ya Kuwait iliamua kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na usafirishaji haramu wa watu ikiwemo kuanzisha kitengo maalumu kwenye wizara ya mambo ya ndani kudhibiti hali hiyo.