Skip to main content

Wakurugenzi wa PAHO na WHO kukutana Brazili kutathimini kukabili virusi vya Zika

Wakurugenzi wa PAHO na WHO kukutana Brazili kutathimini kukabili virusi vya Zika

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani(WHO) Bi Margaret Chan, na mkurugenzi wa Shirika la Afya la Mataifa ya Amerika (PAHO),  Carissa F. Etienne, wanakutana wiki na maafisa wa ngazi za juu wa Brazili akiwemo waziri wa afya Marcelo Castro, kutathimini hali ya virusi vya Zika na jinsi ya kukabiliana navyo.

Katika ziara yao nchini Brazil Dr. Chan na Etienne watakutana na Rais Dilma Rousseff  leo Jumanne na pia watatembelea kituo cha kitaifa cha hatari na udhibiti wa majanga kwa ajili ya kujadili na mawaziri mbalimbali, wakiwemo wa afya na ulinzi.