Ban Ki-moon alaani mashambulizi ya kigaidi Homs na Damascus

Ban Ki-moon alaani mashambulizi ya kigaidi Homs na Damascus

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani mashambulizi ya makombora yaliyofanyika tarehe 21 Februari kwenye maeneo ya Damascus na Homs nchini Syria ambapo kikundi cha kigaidi cha ISIL kimedai kuhusika na mashambulizi hayo.

Taarifa iliyotolewa leo na msemaji wake imeeleza kwamba watu wapatao 155 wameuawa, wengi wao wakiwa ni raia, huku mamia wakiwa wamejeruhiwa.

Katibu Mkuu ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga na kuwatakia nafuu waliojeruhiwa, akiongeza kwamba waliotekeleza mashambulizi hayo ya kigaidi wanapaswa kuwajibisha.