Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka mitano tangu kuzuka mzozo Syria, nchi imesambaratika, raia ndio wanaolipa gharama za vita:UM

Miaka mitano tangu kuzuka mzozo Syria, nchi imesambaratika, raia ndio wanaolipa gharama za vita:UM

Wakati mzozo wa Syria unakaribia kuingia mwaka wa sita , raia ndio wanaolipa gharama za vita vinavyoendesha na pande mbalimbali nchini humo , wakati taifa lao likisambaratika, wanaume ,wanawake na watoto wakishambuliwa, kukimbia makwao na kusaka usalama kila uchao.

Katika ripoti yake mpya tume ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria imetanabaisha uharibifu wa miundombinu, nchini humo uliosababishwa na miaka mitano ya vita ikiwemo huduma za afya na majengo ya elimu, maeneo ya wazi , huduma za umeme na maji.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Paulo Sérgio Pinheiro wanashuhudia  wapiganaji wengi wa n jewakishirikia vita Syria katika pande zote na kuongeza madhila kwa raia na jamii zao.

(SAUTI YA PINHEIRO)

“Matokeo makubwa ya ripoti hii ni kwamba wanaolipa gharama za vita hivi ni raia, kwa sababu pande kinzani haziheshimu sheria za ushiriki wa mapigano. Pia kuna uharibifu mkubwa wa shule na hospitali ni maafa makubwa. Ni ripoti inayotia mashaka sana tuliyoitoa safari hii”

Ameongeza kuwa mashambulizi ya anga yameongezeka na maeneo salama yamepungua, huku maazimio ya Baraza la Usalama yakipuuzwa. Pia maeneo ya urithi wa kitamaduni ambayo yalikuwa muhimu sio kwa Syria tuu bali kwa dunia yamebomolewa na kuharibiwa na mashambulizi ya makusudi na ya bahati mbaya.

Ripoti hiyo pia imeelezea mgawanyiko katika taifa hilo, ongezeko la mashambulizi, maeneo kuzingirwa na mmomonyoko katika suala la kuaminiana baina ya jamii.

Ripoti hiyo imetokana na mahojiano wamashuhuda na raia 415 , maoni yaliyokusanywa kati ya Julai 2015 na Januari 2016. Imebaini uhalifu dhidi ya ubinadamu unaOtekelezwa na vikosi vya serikali na kundi la kigaidi la ISIS. Imesisitiza hatua ya kimataifa ili kupata suluhu ya kisiasa kumaliza vita Syria.