Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia wa DRC wawajibike kuhusu maendeleo ya nchi yao

Raia wa DRC wawajibike kuhusu maendeleo ya nchi yao

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokraisa ya Congo DRC, Maman Sidikou, amewasihi raia wa DRC kuwajibika katika kuendeleza maendeleo ya nchi yao. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzuru maeneo ya Kivu Kaskazini pamoja na Mwakilishi wa kanisa katoliki nchini humo Luis Mariano.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na redio washiria Radio OKAPI, Maman Sidikou amesisitiza pia kwamba Ujumbe wa Umoja wa Mataifa DRC MONUSCO unatarajia kuondoka nchini humo, akiongeza kwamba kabla ya hatua hiyo lazima utulivu wa kudumu urejeshwe nchini DRC.

Kuhusu kurejeshwa kwa ushirikiano baina ya jeshi la kitaifa la DRC na MONUSCO, amesema karibu ushirikiano huo utaanza upya nchini kote.