Yemen iko katika hatihati ya kukabiliwa na janga kubwa waonya UM

Yemen iko katika hatihati ya kukabiliwa na janga kubwa waonya UM

Mapigano nchini Yemen yameiacha nchi hiyo katika hatihati ya janga kubwa, umesema Umoja wa mataifa Ijumaa wakati wa ombi la dola bilioni 1.6 ambazo zinahitajika ili kutoa msaada muhimu kwa watu takribani milioni 8.Jamie McGoldrick, ni mratibu mkazi wa Umoja wa mataifa katika masuala ya kibinadamu nchini huo.

(SAUTI YA McGOLDRICK)

"Mgogoro unaoendelea bado umesalia kama awali. Mashambulizi kutoka ardhini na makombora vile vile kutoka  angani, na hili ni jambo la kawaida katika sehemu nyingi za Yemen, na matokeo ya wakazi wamekuwa katika wakati ngumu.”

Mratibu huyo ameongeza kuwa mashirika ya misaada bado yanakabiliwa na changamoto nyingi kwenda katika baadhi ya sehemu ambazo  hazifikiki nchini Yemen ambako watu zaidi ya milioni 14 sasa wanakabiliwa na uhaba wa chakula.

Kwa ujumla watu milioni 21 wanahitaji msaada wa aina fulani wa kibinadamu nchini humo ambako mapigano baina ya serikali na watu jamii ya Houthi yangalipo, na Umoja wa Mataifa unajitahidi kuleta suluhu ya amani.