Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yapeleka misaada ya dharura kwa watoto Syria

UNICEF yapeleka misaada ya dharura kwa watoto Syria

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF limeelezea kuwa limeshiriki kwenye msafara wa kupelekea misaada ya dharura kwa jamii zilizozingirwa nchini Syria.

Miongoni mwa watu 82,000 waliopatiwa usaidizi kwenye miji ya Madaya, Foah, Kfreya, Moademiyeh na Zabadani, 37,000 walikuwa ni watoto.

Taarifa ya UNICEF imeeleza kwamba vifaa vilivyotolewa ni pamoja na vyakula maalum kwa ajili ya watoto wanaokumbwa na utapiamlo, vitamini na dawa za kutibu upungufu wa damu, ugonjwa wa kuhara na minyoo,

Kwa mujibu wa Mwakilishi wa UNICEF nchini Syria, Hanaa Singer, lengo la shirika hilo ni kuongeza kasi ya kupeleka misaada ili kuweza kuwafikia watoto zaidi ya milioni mbili wanaohitaji msaada kwa haraka.

Halikadhalika UNICEF imeanza kupeleka huduma za maji kwenye mji wa Aleppo ambapo miundumbinu imeharibika, ikitoa lita milioni 8 za maji kila siku.