Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNMISS yalaani vikali ghasia katika kituo cha ulinzi wa raia Malakal

UNMISS yalaani vikali ghasia katika kituo cha ulinzi wa raia Malakal

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS, umelaani vikali ghasia zilizozuka jana usiku kati ya vijana wa makabila ya Shilluk na Dinka kwenye kituo chake cha ulinzi wa raia kwenye mji wa Malakal. Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Kwa mujibu wa UNMISS, ghasia hizo zimeendelea hadi leo Alhamis tarehe 18 asubuhi. UNMISS imetoa wito kwa jamii zote zijiepushe na machafuko, zirejeshe utulivu na kutatua mizozano yao kwa njia ya mazungumzo.

Duru za habari zinasema raia watano wakimbizi wa ndani waliuawa na wengine wapatao 30 kujeruhiwa katika ghasia hizo zilizozuka jana jioni, kati ya vijana wa makabila hayo mawili.

UNMISS imekumbusha wahusika wote kwamba mashambulizi dhidi ya kituo cha ulinzi wa raia na majengo ya Umoja wa Mataifa yanaweza kuwa uhalifu wa kivita.