Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda yaamua Februari 18, ni Rais na wabunge

Uganda yaamua Februari 18, ni Rais na wabunge

Nchini Uganda, tarehe 18 Februari mwaka 2016 ni siku ya uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge. Kampeni zimefikia ukingoni kila mgombea akijinasibu kuibuka mshindi ambapo matokeo yanatarajiwa kutangazwa siku tatu baada ya uchaguzi. Je maandalizi yamekuwa vipi? Matumaini ya wananchi ni yapi katika uchaguzi huo wa Rais ambapo kipindi cha Urais hakina ukomo? Mwandishi wetu kutoka Uganda, John Kibego amevinjari huko Hoima kuzungumza na wananchi.