Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA na kituo cha Lajee wamezindua maeneo ya kuchezea watoto kwenye kambi ya Aida

UNRWA na kituo cha Lajee wamezindua maeneo ya kuchezea watoto kwenye kambi ya Aida

Leo shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Palestina UNRWA na kituo cha Lajee  wamezindua kwa mara ya kwanza kabisa maeneo ya kuburudisha watoto ikiwemo uwanja wa mpira wa miguu kwenye kambi ya wakimbizi ya Aida mjini Bethlehem.

Kupatikana kwa maeneo hayo ya watoto kumewezeshwa na mchango kutoka ofisi ya Umoja wa Mataifa ya michezo kwa maendeleo na amani (UNOSDP) na yatawapa watoto wa kambi ya Aida fursa ya nadra ya kucheza na kujipatia marafiki katika mazingira hayo magumu.

Kamishina mkuu wa URWA Pierre Krähenbühl, mkurugenzi wa operesheni wa UNRWA ukingo wa Magharibi Felipe Sanchez; waziri wa mambo ya nje wa Iceland, Gunnar Bragi Sveinsson, mkurugenzi wa kituo cha Lajee, Salah Ajarma; wanadiplomasia kutoka nchi mbalimbali na wawakilishi wa jamii wameshiriki uzinduzi huo.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa UNRWA maeneo hayo ni muhimu saana kwa maisha na mustakhbali wa watoto katika kambi ya Aida.