Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la kimataifa kuhusu teknolojia na vinasaba katika kilimo limehitimishwa

Kongamano la kimataifa kuhusu teknolojia na vinasaba katika kilimo limehitimishwa

Takriban washiriki 500 wakiwemo wanasayansi , wawakilishi wa serikali, jumuiya za kijamii, sekta binafsi, wanazuoni na makampuni wameshiriki kongamano la kimataifa kuhusu teknolojia za kibaolojia na vinasaba  katika kuinua kilimo lililohitimishwa leo mjini Rome Italia.

Kongamano hilo lilioandaliwa na shirika la kilimo na chakula FAO limejadili teknolojia hizo kwa manufaa ya wakulima hususani wadogowadogo kutoka katika mataifa yanayoendelea.  Graziano da Silva ni mkurugenzi mkuu wa FAo akizungumza wakati wa kufunga kongamano hilo amesema

(SAUTI YA GRAZIANO)

'Tumefungua mlango, tulianzisha mjadala na sasa tunaona ni jinsi gani kilimo na  teknolojia za kibayolojia zinaweza kushirikishwa, na ni vipi zitumike pamoja, Nadhani hii ni hatua muhimu ya kuzingatia kwani inafungua fursa kwa ajili ya uimarishaji wa teknolojia mpya ambayo itaimarisha uendelevu wa sekta ya kilimo katika miaka ijayo."