Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fursa ya misaada ya kibinadamu yajadiliwa na de Mistura na serikali ya Syria

Fursa ya misaada ya kibinadamu yajadiliwa na de Mistura na serikali ya Syria

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya Syria Bwana Stefan de Mistura amehitimisha mkutano wake na waziri wa mambo ya nje wa Syria Walid Al Moalim mjini Damascus.

Miongoni mwa waliyojadili  viongozi hao wawili ni kutoa fursa kwa misaada ya kibinadamu kuingia katika maeneo yyote yanayozingirwa na vikosi vya upinzani, serikali na kundi la ISIL.

Bwana de Mistura amesema maelfu ya watu wanakufa na njaa na wengine kwa kukosa matibabu kwa kuwa misaada muhimu ya kibinadamu haiwezi kuwafikia kutokana na mapigano na maeneo waliyopo kutofikiwa na wahudumu wa misaada.

Leo anatarajiwa kuwa na mkutano mwingine kama anavyofafanua msemaji wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva Ahmed Fawzi.

(SAUTI YA AHMED FAUWZI)

Watakuwa na mkutano mwingine leo Syria kushughulikia sula hili la haraka, ambalo linahusiana na mustakhbali wa Wasyria wote na ambalo linahusiana na ahadi na hitimisho na muafaka wa Munic.”