Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatma ya mji mkongwe Zanzibar kufahamika juma lijalo: UNESCO

Hatma ya mji mkongwe Zanzibar kufahamika juma lijalo: UNESCO

Jopo la wataalamu wa mazingira kutoka makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO linatarajiwa kuwasili kisiwani Zanzibar nchini Tanzania mwishoni mwa juma,  kufanya majadiliano na mamlaka visiwani humo kuhusu hatma ya mji mkongwe ambao uliwekwa katika orodha ya maeneo yaliyo hatarini kuondolewa kwenye orodha ya urithi wa dunia.

Katika mahojiano na idhaa hii, Katibu Mtendaji wa tume ya taifa ya UNESCO nchini Tanzania Dk Moshi Kimizi amesema baada ya majadiliano ya muda mrefu jopo hilo sasa litakutana na pande husika ambazo ni serikali na mamlaka ya UNESCO akisema mjadala utahusu.

(SAUTI DK KIMIZI)

Hata hivyo Dk Kimizi amesema ana matumaini kuwa muafaka utafikiwa ili kulinda hadhi ya mji huo muhimu kwa hostoria ya Afrika Mashariki.