Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hukumu dhidi ya raia wa kigeni waliolazimishwa kukiri makosa UAE yalaaniwa

Hukumu dhidi ya raia wa kigeni waliolazimishwa kukiri makosa UAE yalaaniwa

Kundi la wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa leo wameitaka serikali ya Umoja wa nchi za Kiarabu UAE, kuheshimu haki za msingi za raia kadhaa wa kigeni ambao inawashikilia kwa mwaka mmoja na nusu sasa na kuitolea wito kuwaachilia mara moja bila masharti yeyote.

Salim Alaradi, raia wa Canada mwenye asili ya Libya, Kamal Ahmed Al Darrat na Mohamed Kamal Al Darrat, ambao ni baba na mwana wote raia wa Marekani wenye asili ya Libya, Adel Rajab Beleid Nasef na Moad Mohamed Al Hashmi, wote raia wa Libya walikamatwa na maafisa usalama wa serikali tangu Agosti mwaka 2014.