Redio yaelimisha jamii kuhusu malaria DRC

Redio yaelimisha jamii kuhusu malaria DRC

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Radio washirika Umoja imejitahidi kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa malaria uliokithiri kwenye eneo la Fizi, Kivu Kusini.

Kupitia programu mbali mbali redio hiyo imetoa mafunzo kwa wananchi kuhusu jinsi ya kujikinga na mbu na kuzuia maambukizi ya malaria. Wasikilizaji wamenufaika na mafunzo hayo, kadhalika viongozi wa sekta ya afya hadi visa vya malaria vikaanza kupungua, hii kiwa ni ishara ya umuhimu wa redio katika kuokoa maisha wakati huu dunia ikiwa imeadhimisha siku ya kimataifa ya redio hivi karibuni.

Kulikoni ? Ungana na Langi Stan Assumani wa radio washirika Radio Umoja kwenye makala hii.