Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha uchaguzi wa Rais wa mpito Haiti

Ban akaribisha uchaguzi wa Rais wa mpito Haiti

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amekaribisha uchaguzi wa Februari 14 uliofanywa na bunge la kitaifa la Haiti kumchagua Rais wa mpito wa nchi hiyo. Uchaguzi huu unatokana na mkataba uliosainiwa tarehe 6 Februari kati ya wadau wa Haiti ili kuhakikisha muendelezo wa taasisi za serikali na mchakato zaidi wa uchaguzi.

Akikaribisha hatua hiyo muhimu ya kwanza , Katibu Mkuu amezichagiza pande zote kufanya kazi pamoja kuelekea utekelezaji wa mpango ulioainishwa katika muafaka ili kuhakikisha kurejea kwa utawala wa katika hali ya kawaida.

Katibu Mkuu ameelezea kujiamini kwake kwamba kurejesha utulivu Haiti na mchakato wa demokrasia vitaendelea kwa njia ya amani na mshikamano.