Mustakhbali wa ushirikiano wa kimataifa wa shughuli za anga wajadiliwa

15 Februari 2016

Uendelevu wa muda mrefu wa shughuli za anga itakuwa moja ya mada muhimu katika kikao 53 cha Sayansi na Ufundi cha kamati ndogo ya amani na matumizi ya anga (COPUOS), kilichoanza leo kwenye Umoja wa Mataifa mjini Vienna.

Vitu vingine muhimu vitakavyojadiliwa na mkutano huo ni pamoja na kukabiliana na uchafu angani, matumizi ya zana za angani kwa ajili ya usimamizi wa majanga na maendeleo ya hivi karibuni katika matumizi ya vyombo vya kupimia dunia kwa njia ya satelaiti kusaidia utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu.Matumizi salama ya vyanzo vya nguvu za nyuklia katika anga, utafiti wa hali ya hewa angani na matumizi ya obiti geostationary, pamoja na mifumo ya kimataifa ya urambazaji satellite.

Hatua muhimu kwa kamati ilikuwa ni kuanza rasmi kwa mchakato wa  'UNISPACE + 50' mwaka 2015, ambao utaweza kuongoza mustakhbali wake katika utawala anga ya kimataifa.' UNISPACE + 50" itaadhimisha miaka 50 ya mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kuhusu utafiti na matumizi ya amani ya anga ifikapo  2018, (UNISPACE I), uliofanyika mjini Vienna mwaka 1968.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter