Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi zaidi zahitajika kupambana na saratani utotoni- IARC

Juhudi zaidi zahitajika kupambana na saratani utotoni- IARC

Takwimu mpya za Shirika la Kimataifa la Utafiti katika Saratani, IARC, zimeonyesha kuwa visa vya saratani miongoni mwa watoto sasa ni vingi kuliko ilivyodhaniwa zamani.

IARC, ambayo ni kitengo cha Shirika la Afya Duniani, WHO, imesema hayo leo, ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya Saratani Utotoni, ikiongeza kuwa juhudi zaidi zinahitajika katika kupambana na saratani ya utotoni.

Ingawa saratani ni adimu miongoni mwa watoto kote duniani, inakadiriwa kuwa visa 215,000 vya saratani hugundulika kila mwaka miongoni mwa watoto chini ya umri wa miaka 15, na takriban visa 85,000 miongoni mwa barubaru kati ya miaka 15 na 19.

Makadirio haya yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa zaidi ya sajili 100 za saratani katika nchi 68 duniani, kati ya 2001-2010.