Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kazi ya kuhesabu kura nchini CAR yaendelea - MINUSCA

Kazi ya kuhesabu kura nchini CAR yaendelea - MINUSCA

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR , kazi ya kuhesabu kura inaendelea kufuatia duru ya pili ya uchaguzi wa rais na awamu mpya ya uchaguzi wa wabunge iliyofanyika Jumapili hii  kwa msaada mkubwa wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSCA> Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Sauti za wafanyakazi wa Tume ya Kitaifa ya uchaguzi nchini CAR wakihesabu kura baada ya uchaguzi uliofanyika jumapili hii nchini humo.

Walinda amani wa MINUSCA wameshiriki maandalizi na uratibu wa uchaguzi huo, wakiwa wamesaidia kuhakikisha masanduku ya kura yanafungwa rasmi na kusafirishwa kwa usalama kwenye mji mkuu Bangui.

Kwenye video iliyotolewa na MINUSCA, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa MAtaifa nchini humo, Parfait ONanga Anyanga alizungumza baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa..

(Sauti ya Bwana Onanga Anyanga)

“Ukweli utajulikana wakati wa kuhesabu kura. Na lazima zoezi hili lifanyike haraka, ili lisifanyike wakati wa usiku, kwa sababu matatizo ya umeme yanaweza kuzuia utekelezaji mzuri wa kuhesabu za kura. Lakini nadhani maandalizi yote yamefanyika, tumehakikisha vituo vyote vimepatiwa na tochi.