Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamano la matumizi y ya mifumo ya viumbe kwa ufanisi wa chakula laanza Roma:FAO

Kongamano la matumizi y ya mifumo ya viumbe kwa ufanisi wa chakula laanza Roma:FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO limeo limeanza kongamano la kimataifa la siku tatu kuhusu matumizi ya michakato ya kibayolojia na mifumo ya viumbe kwa ajili ya mifumo endelevu ya chakula na lishe.

Kongamano hilo linawaleta pamoja wataalamu kutoka kila pembe ya dunia litadodosa jinsi gani michakato ya kibayolojia na mifumo ya viumbe inaweza kunufaisha wakulima wadogowadogo hususani walio katika nchi zinazoendelea zilizoathirika na mabadiliko ya tabianchi , ongezeko la idadi ya watu na masuala mengine ya kijamii na kiuchumi. Dr Ren Wang ni mkurugenzi mkuu msaidizi wa idara ya kilimo na matumizi ya FAO

(SAUTI YA REN WANG)

"FAO inatambua umuhimu wa mazoa yanayokuzwa kwa kutumia marekebisho ya kijenetiki, GMO, katika kuimarisha mazao hususan katika mazingira hatarishi, FAO vile vile inatambua hatari zinazoendana na teknolojia hizi mpya na FAO ingependa kuhimiza wakulima na serikali na mashirika ya utafiti kuangalia kwa kina umuhimu na changamoto za teknolojia hizo."