Skip to main content

UM wagawa chakula na msaada mwingine kwa wakimbizi wa ndani 38,000 Darfur

UM wagawa chakula na msaada mwingine kwa wakimbizi wa ndani 38,000 Darfur

Umoja wa Mataifa na washirika wake wamekuwa wakigawa msaada wa chakula na misaada mingine ya kibinadamu kwa raia 38,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto waliotawanywa na mapigano ya karibuni kwenye eneo la Jabel Mara Darfur. Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Msaada mwingine wa kuokoa maisha uliowasilishwa na malori ya mpango wa pamoja wa Umoja wa mataifa na Muungano wa Afrika wa kulinda Amani Darfur UNAMID ni pamoja na maji, malazi, vifaa vya kupikia, vyoo, madawa na lishe kwa watoto walio na utapia mlo.

Mapigano kwenye eneo la Jebel Marra, yaliyoshika kasi katikati ya mwezi Januari yamewafungisha virago maelfu ya raia katika eneo hilo la milimani huku wengi wao wakitembea mwendo mrefu bila chakula wala maji.

Watu 38,000 waliopokea msaada wa chakula wako katika maeneo matatu ya Kaskazini mwa Darfur, Sortoni,Tawilla  kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani na  katika mji wa Kebkabiya .