Akiwa Canada, Ban azungumzia kuzuia itikadi kali katili

13 Februari 2016

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema leo kuwa kujikita katika kuzuia itikadi kali katili ni muhimu sana, kwani hilo ni moja ya matishio makubwa zaidi dhidi ya dunia enzi za sasa.

Ban amesema hayo akiwa kwenye kituo cha kuzuia uenezaji wa itikadi kali zinazochangia ukatili, jijini Montreal, Canada, akiongeza kuwa jitihada hizo zinahitaji kuwa bunifu, fanisi na zenye utu.

Katibu Mkuu amesema kuwa amefanya kuzuia itikadi kali katili kuwa suala la kipaumbele kwa Umoja wa Mataifa, na kwamba ndiyo maanda aliwasilisha mkakati mpya wa kuchukua hatua kuzuia itikadi kali katili mwezi uliopita kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambao unasisitiza umuhimu wa kushughulikia vyanzo vya itikadi katili.

Aidha, Ban amesema ni lazima ni lazima kuwezesha uwiano baina ya amani na usalama, maendeleo endelevu, haki za binadamu na wadau wa kibinadamu kwenye ngazi zote, ikiwemo katika Umoja wa Mataifa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter