Mambo yanayoendelea katika himaya ya Palestina na Israel yanatia hofu:UM

Mambo yanayoendelea katika himaya ya Palestina na Israel yanatia hofu:UM

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema inatiwa hofu na maendeleo ya karibuni katika himaya ya Palestina na Israel. Ofisi hiyo inasema imepokea taarifa za kuogofya kwamba kikosi cha Qassam kimemuua mmoja wa wanachama wake kwenye Ukanda wa Gaza mnamo Februari 7.

Bwana Mahmoud Ishtewi ameripotiwa kushikiliwa kwa miezi kadhaa na kikosi cha Qassam bila mchakato wowote wa kisheria kwa madai ya utovu wa nidhamu. Kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu kuna taarifa za kuaminika kuwa hakutendewa haki akiwa kizuizini.

Ofisi ya haki za binadamu pia inahofia hali ya bwana Mohammad Al-Qiq, Palestina aliye kwenye mgomo wa kula kwa siku 80 akipinga kushikilia kizuizini nchini Israel wakitana ama afunguliwe mashitaka au aachiliwe mara moja.