ESCAP yatoa wito wa kuboresha ushirikiano wa kikanda kufikia malengo ya SDG’s Asia ya Kati na Kaskazini:

ESCAP yatoa wito wa kuboresha ushirikiano wa kikanda kufikia malengo ya SDG’s Asia ya Kati na Kaskazini:

Msaidizi wa Katibu Mkuu na Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Uchumi na Jamii kwa Mataifa ya Asia na Pacific, ESCAP Dr. Shamshad Akhtar amekutana na Rais wa Turkministan Bwana Gurbanguly Berdimuhamedow, alipokuwa akihitimisha ziara yake katika mataifa matano ya Kaskazini na Katikati mwa Asia, iliyokuwa na lengo la kuimarisha ushirika baina ya ESCAP na wanachama wake.

Ziara ya wiki mbili ya Dr. Akhtar imejumuisha kukutana na Rais wa Armenia, Azerbaijan, waziri mkuu wa Kazakhstan na Rais wa Tajikistan,pamoja na mawaziri wengine, magavana wa Benki, wanazuoni na wawakilishi wa sekta binafsi kujadili hali ya sasa ya kiuchumi katika eneo la Kaskazini na Asia ya Kati.

Wakati wa majadiliano na viongozi Dr. Akhtar amesisitiza haja ya kuimarisha ushirikiano na mshikamano wa kiuchumi wa kikanda ili kufikia malengo mapya ya maendeleo endelevu SDG’s na kuongelea kipaumbele cha mkutano ujao wa viongozi wa Asia ya Kati na Kaskazini utakaofanyika Bangkok May 17, mwaka huu kama sehemu ya kikao cha 72 cha ESCAP.