Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya mitandao ya kijamii , hakuna mbadala wa redio: Adama Dieng

Licha ya mitandao ya kijamii , hakuna mbadala wa redio: Adama Dieng

Kuelekea siku ya redio duniani Februari 13, Mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari Adam Dieng amesema hakuna mbadala wa chombo hicho adhimu na kuzungumzia wajibu wake muhimu wakati wa mizozo.

Katika mahojiano maalum na redio ya Umoja wa Mataifa Bwana Dieng amesema licha ya uwepo wa mitandao ya kijamii na televisheni lakini bado redio inaendelea kuwa chombo kinachoweza kuwafikia watu wengi hususani katika dhiki.

Akitolea mfano wa mizozo anasema.

(SAUTI DIENG)

‘‘Hebu fikiri wakati huu ambapo kuna wimbi kubwa la mahitaji ya kibinadamu tunalolishuhudia, nazungumzia mamilioni ya Wasyria wanaolazimika kukimbia makwao, pia akina mama ambao wanahatarisha maisha yao kuvuka bahari kwa ajili ya watoto wao. Katika makundi kama haya utampata mmoja wao ana redio.’’

Akizungumiza maadhimisho ya miaka 70 ya redio ya Umoja wa Mataifa kiongozi huyo amesema inaendelea kukumbusha maneno ya awali ya katiba ya Umoja wa Mataraifa iliyosainiwa mjini San Francisco.