Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika azuru Gabon

Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika azuru Gabon

Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti, yupo mjini Libreville, Gabon, kwa ziara ya siku tano, ambapo pia anashiriki katika kongamano la saba la Mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Kati, ambalo limeanza leo Ijumaa Februari 12.

Katika awamu ya kwanza ya ziara yake hiyo, Dkt. Moeti amemtembelea Rais Ali Bongo Ondimba, ambaye amemsifu kwa kutoa kipaumbele kwa afya katika ajenda ya maendeleo ya Gabon.

Amesifu uongozi wa rais huyo, pamoja na kutambua mchango wa Gabon katika kuelekea kufikia huduma ya afya kwa wote, kupitia mfumo wake wa kitaifa wa riba ya afya, ambao unawasaidia watu maskini na walio wanyonge kupata huduma bora ya afya.

Amesema mfumo huo ni mfano wa ufanisi unaopaswa kuigwa na nchi zingine katika kanda ya Afrika, zinapofanya jitihada za kuwezesha huduma ya afya kwa wote.