Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya magumu wanayopitia maelfu bado wanafunga safari kuingia Ulaya:UNHCR

Licha ya magumu wanayopitia maelfu bado wanafunga safari kuingia Ulaya:UNHCR

Zaidi ya wakimbizi na wahamiaji 80,000 wamewasili Ulaya kwa njia ya boti katika wiki sita za mwanzo wa mwaka huu na wengine zaidi ya 400 kupoteza maisha yao wakijaribu kuvuka bahari, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Likiongeza kuwa licha ya kuchafuka kwa bahari, baridi kali na magumu mengi wanapowasili, bado wakimbizi na wahamiaji 2000 kwa siku wanajitosa katika hatari inayohatarisha maisha yao nay a watoto wao ili kuingia Ulaya.

Ufumbuzi kwa hali ya Ulaya si kwamba tu inawezekana, lakini tayari mataifa yamekubaliana na kuna haja ya haraka ya kutekelezwa.  UNHCR imesema udhibiti ni muhimu na ni jambo ambalo pia linahitajika na umma kama anavyofafanua Melisa Flemming msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA MELISA FLEMMING)

“Kuna umuhimu wa hatua za pamoja na madhubuti kutoka nchi za Ulaya. Vile vile tuna wasiwasi kutokana na ongezeko la chuki na mashambulizi dhidi ya wahamiaji wanaoingia Ulaya.”