Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Radio ni njia muhimu ya kuwasilisha habari katika majanga: ITU

Radio ni njia muhimu ya kuwasilisha habari katika majanga: ITU

Leo ikiwa ni siku ya Radio duniani, Shirika la Umoja wa mataifa la muunganoi wa kimataifa wa mawasiliano ITU limekumbusha jukumu la Radio katika udhibiti na kukabiliana na hali kabla na baada ya majanga.

Kwa mujibu wa ITU, Radio inatambulika kuwa ni njia ya gharama nafuu ya mawasiliano ambayo inafika hata vijijini na hususani huweza kuwafikia waathirika wa majanga wakati njia zingine za mawasiliano zimeathirika.

ITU imeongeza kuwa matangazo ya Radio ni muhimu saana kwa kufikisha taarifa kwa wakati, zinazohitajika na za muhimu kwa watu ambao wamepatwa na taharuki na kukatishwa tamaa na athari za majanga .

Imeongeza kuwa kutoa taarifa kwa waathirika kupitia Radio ni muhimu sana hasa pale ambapo hapafikiki na watoa misaada wanaweza kuchukua sikui nyingi au wiki kadhaa kufikia jamii zilizoathirika .

Akitia msisitizo kuhusu hilo Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon amesema majanga yanayosababishwa na binadamu au ya asili yote ynaitia hofu jumuiya ya kimataifa , na pindi yakizuka na kuwa na dharura basi Radio inaweza kuwa mkombozi wa maisha.