Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utafiti wa Zika unaendelea haraka: WHO

Utafiti wa Zika unaendelea haraka: WHO

Uelewa mdogo wa virusi vya Zika umetoa changamoto katika suala zima la maendeleo ya utafiti , lakini hata hivyo kutokana na uzoefu katika masula ya utafiti wakati wa mlipuko wa Ebola Afrika Magharibi shirika la afya duniani WHO linasema utafiti kukabilina na Zika unaendelea haraka sana.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis Dr Marie-Paule Kieny, mkurugenzi mkuu msaidizi wa mifumo ya afya na ubunifu wa WHO amesema , baada ya Ebola WHO ilianza kuandaa mpango kabambe wa kujiandaa na dharura ya afya na kuwa na uwezo wa kufanya utafiti haraka pale inapohitajika. Lengo ni kuhakikisha upatikanaji wa hatua za kitabibu za kukabiliana na mlipuko , lakini pia kudhibiti athari zake. Ameongeza

(SAUTI YA DR MARIE-PAULE KIENY)

“Tayari tumeshabaini idadi kubwa ya wazalishaji na taasisi za utafiti ambazo ama zinashiriki katika maendeleo ya zana matibabu ya Zika, au zina nia ya kujiingiza katika utafiti huo"