Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nigeria ihakikishe maeneo iliyoyakomboa toka Boko Haram kweli ni salama: UM

Nigeria ihakikishe maeneo iliyoyakomboa toka Boko Haram kweli ni salama: UM

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa leo wameitaka serikali ya Nigeria kuhakikisha kwamba maeneo inayosema imeyakomboa kutoka kwa majeshi ya Boko Haram kweli ni salama kwa wakimbizi wa ndani waliotawamnywa na mapigano kuweza kurejea nyumbani.

Pia wametoa wito wa makambi yote , rasmi na yasiyo rasmi ya wakimbizi wa ndani kulindwa na kusisitiza kwamba watu watu wanaorejea iwe ni kwa hiyari na utaratibu maalumu.

Wito huo umekuja baada ya mfululizo wa mashambulizi ya Boko Haram katika vijiji Kaskazini mwa Nigeria, ambayo yanajumuisha jaribio la kuvamia kambi ya wakimbizi wa ndani karibu na kijiji cha Dalori, ambako inasemekanazaidi ya watu 90 wengi wao wanawake na watoto wameuawa.

Wataalamu hao wamesema kwa mujibu wa taarifa siku ya Jumanne wanawake wawili waliokuwa na vilipuzi walijitoa mhanga na kushambulia eneo la wakimbizi wa ndani raia wa Nigeria la Dikwa, na kuuwa watu zaidi ya 50 na wengine wengi kujeruhiwa.

Hivyo wameitaka serikali ya Nigeria kupanga kwa uangalifu mipango yoyoye ya wakimbizi wa ndani kurejea nyumbani wakizingatia hatari ya mashambulizi ya Boko Haram.