Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viwango vya UNECE vyaisaidia Namibia kusafirisha zabibu Ulaya:

Viwango vya UNECE vyaisaidia Namibia kusafirisha zabibu Ulaya:

Kwa mara ya kwanza mwezi Desemba mwaka jana makasha au makontena yaliyobeba zabibu yaliondoka katika bandari ya Lüderitz, Namibia, kuelekea Ulaya na yote yakiwa katika ubora wa viwango vya kilimo vilivyowekwa na tume ya Umoja wa mataifa ya maendeleo kwa ajili ya Ulaya UNECE.

Zabibu hizo zimekuwa ndio zao la kwanza kusafirishwa moja kwa moja kutoka Nabia hadi kwenye Muungano wa Ulaya, wakatio usafirishaji huo ni jambo la kawaida kwa nchi jirani ya Afrika ya Kusini. Kwa Namibia kufanikiwa kussafirisha zabibu hizo na kufanikiwa kufikia ubora na viwango vilivyowekwa ni hatua kubwa kuelekea siku za usoni.

Namibia ambayo theluthi mbili ya watu wake milioni 2.4 wanategemea kilimo kwa njia moja au nyingine sasa inatafiti zaidi jinsi ya kusaidia usafirishaji nje wa bidhaa zingine za kilimo na pia kutafakari uingizaji wa bidhaa kutoka mataifa mengine ya Afrika.