Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

El Niño kuathiri vibaya mavuno na usalama wa chakula Kusini mwa Afrika:FAO

El Niño kuathiri vibaya mavuno na usalama wa chakula Kusini mwa Afrika:FAO

Eneo la Kusini mwa Afrika liko katika hatihati ya kukabiliwa na ukame ambao umeongezeka tangu mwanzo wa msimu wa kilimo wa 2015-2016 na kuchochewa na matukio makubwa ya El Niño kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 50 iliyopita. Amina Hassan na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Amina)

Kwa mujibu wa FAO ,maeneo ya Zimbabwe, Malawi, Zambia, Afrika Kusini, Msumbiji, Botswana, na Madagascar, hivi sasa yanashuhudia kiwango kidogo kabisa cha mfua kuwahi kutokea kwa miaka 35.

Maeneo ya kilimo ya Kaskazini mwa Namibia na Kusini mwa Angola pia yanakabiliwa na uhaba wa mvua na maji.

FAO inasema maeneo mengi ya Kusini mwa Afrika yameshuhudia kuchelewa kwa msimu wa upanzi na hali mbaya ya kuota kwa mazao, huku maeneo mengine yakichelewa kati ya siku 30 hadi 50.

Utabiri unaashiria kwamba kutaendelea kuwa na uhaba wa mvua na ongezeko la joto katika ukanda mzima na hivyo kusababisha kuporomoka kwa uzalishaji wa mazao katika mwaka huu wa 2016.