Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Radio ni daraja kati ya shughuli za UM na ulimwengu- Dkt. Asha-Rose

Radio ni daraja kati ya shughuli za UM na ulimwengu- Dkt. Asha-Rose

Aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Asha-Rose Migiro amesema miaka 70 ya Radio ya Umoja wa Mataifa imedhihirisha jinsi chombo hicho cha upashaji habari kilivyo daraja kati ya Umoja huo na ulimwengu.

Akihojiwa na Idhaa hii kuadhimisha  siku ya radio duniani sambamba na miaka 70 ya Radio ya Umoja wa Mataifa Dkt. Asha-Rose amesema ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na wabia wake umeimarika pia kutokana na  uwepo wa radio

(Sauti ya Asha Rose 1)

Akatolea mfano jinisi umhimu wa radio ya Umoja wa Mataifa ulivyodhihirika katika kukabiliana na janga la tetemeko kubwa la ardhi nchini Haiti na….

(Sauti ya Asha Rose 2)