Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za wahanga wa ugaidi zamulikwa

Haki za wahanga wa ugaidi zamulikwa

Mkutano wa kimataifa kuhusu haki za binadamu za wahanga wa ugaidi umefanyika mjini New York, Marekani ambapo wawakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na mashirika mbalimbali wamejadili dhana hiyo muhimu katika kukabiliana na ugaidi ambalo ni janga la kimataifa.

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa mkutano huo mkuu wa kikosi cha utekelezaji wa makabiliano dhidi ya ugaidi katika Umoja wa Mataifa Jehangir Khan amesema mkutano huu unamulika wahanga wa ugaidi ukiangaza sio tu waliokufa bali hata waliosalia matahalani jamii zao.

Bwana Khan amesema mkutano huo unafanyika wakati muhimu ikiwa ni siku moja kabla baraza kuu la UM halijakutana kujadili mpango mkakati wa Katibu Mkuu kuhusu makabiliano dhidi ya ugaidi .

Amesisitiza moja ya hoja muhimu katika kuwasaida wahanga wa ugaidi.

( SAUTI KHAN)

‘Wakati wahanga wa ugadi wanateseka baada ya shambulio, tunahitaji kuangalia rasilimali gani tunaweza kuzitumia kujenga upya maisha yao.’’