Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuelekea #UNGASS2016 kuhusu madawa ya kulevya, Tanzania yaanza kujipanga

Kuelekea #UNGASS2016 kuhusu madawa ya kulevya, Tanzania yaanza kujipanga

Nchini Tanzania siku ya Jumatano kumefanyika kongamano la wadau wa harakati za kukabiliana na tatizo la madawa ya kulevya. Kongamano hilo limefanyika ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ushiriki wa nchi hiyo kwenye kikao maalum cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu tatizo la madawa ya kulevya duniani, UNGASS kitakachofanyika mwezi Aprili mwaka huu jijini New York, Marekani.

Kongamano hilo liliitishwa na mamlaka ya kitaifa ya udhibiti wa madawa ya kulevya nchini humo, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya udhibiti wa madawa ya kulevya na uhalifu, UNODC nchini Tanzania, ilikuwa mmoja wa waalikwa ambapo Afisa mradi wa kitaifa Immaculate Malyamkono amezungumza na Assumpta Massoi wa Idhaa hii na kumueleza kile ambacho kimejadiliwa na mwelekeo wa baadaye.

Kwanza anaanza na kwa nini mamlaka hiyo ya kitaifa au Drug control and enforcement authority iliitisha kikao hicho.