Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tusake mbinu mbadala kujikwamua na tatizo la madawa ya kulevya: Ban

Tusake mbinu mbadala kujikwamua na tatizo la madawa ya kulevya: Ban

Kuelekea kikao maalum cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu tatizo la madawa ya kulevya duniani baadaye mwaka huu, UNGASS, Katibu Mkuu wa Umoja huo Ban Ki-moon amesema madawa hayo yamekuwa kichocheo cha ghasia, yanakwamisha maendeleo na kutishia ustawi wa jamii.

Akizungumza kwenye kikao cha wadau jijini New York, Marekani Ban amesema mzigo wa madhara wa matumizi yake siyo tu ni kwa wanaoatumia bali pia familia na marafiki zao, halikadhalika mifumo ya afya ambayo inalazimu kuhaha kuwatibu hivyo ametaka ushirikiano ili kupatia suluhu na tiba.

Kwa mantiki hiyo akatoa wito kwa serikali na mashirika ya kiraia..

“Yawe na mjadala mpana kwa kadri iwezekanavyo wakati wa kikao hicho maalum cha tatizo la madawa ya kuleva ili kuangalia mbinu zote za kukwamuka ikiwemo adhabu mbadala kwa makosa madogo, kupanua wigo wa matumizi ya dawa za kupunguza maumivu na machungu kwa waathirika wa madawa ya kulevya, na kuendeleza mbinu mbadala za kujipatia kipato kwa wakulima wa madawa hayo walio hatarini na familia zao.”

Nchini Tanzania nako kumefanyika kikao cha wadau kuelekea UNGASS ambapo Afisa miradi wa kitaifa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kudhibiti madawa ya kulevya na uhalifu, UNODC Immaculate Malyamkono amesema wamejadili mapendekezo kadhaa kukabili hali hiyo ikiwemo..

(Sauti ya Immaculate)