Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID Redio hupatanisha na kuokoka maisha: Jumbe

UNAMID Redio hupatanisha na kuokoka maisha: Jumbe

Tukielekea katika maadhimisho ya Siku ya Redio duniani ambayo mwaka huu maudhui yake ni umuhimu wa chombo hiki cha habari wakati wa majanga, redio ya ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika jimboni Darfur nchini Sudan UNAMID, imesema inatumia vyema uwepo wake kuokoa maisha.

Mkuu wa UNAMID Redio Jumbe Omari Jumbe ameiambia idhaa katika mahojiano maalum kuwa chombo hicho hutekeleza dhana ya urari kwa pande zote kujadiliana na akaongeza.

(SAUTI JUMBE)

Mkuu huyo wa UNAMID amesisitiza umuhimu wa uhuru wa chombo cha habari hususani redio katika kutekeleza majukumu yake.

( SAUTI JUMBE)