Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa dharura wahitajiaka Sudan Kusini: Owusu

Msaada wa dharura wahitajiaka Sudan Kusini: Owusu

Mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini Sudan Kusini Eugene Owusu, ametaka uchangishaji fedha wa dharura ilikuwezesha mashirika ya misaada kutoa misaada wakati wa majira ya kiangazi. Taarifa kamili na Joshua Mmali.

(TAARIFA YA MMALI)

Katika taarifa yake Bwana Owusu amenukuliwa akisema kuwa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wana muda mfupi wa kuyafikia maeneo ambayo yalikatishwa misaada kutokana na mvua na mapigano.

Ameonya kuwa misaada hiyo inapaswa kuwafikia kabla ya kipindi cha mvua kijacho na kwamba ikiwa hatau hiyo haitafanyika sasa hali itakuwa mbaya zaidi.

Tayari kaisi cha zaidi ya dola milioni 20 kimeelekezwa kupitia mfuko wa misaada ya kibiandamu nchini Sudan Kusini CHF wakati kiasi cha dola milioni 220 kikihitajika ilikuchukua hatua ya kimisaada kabla ya mwezi Mei.

Akizungumzia hatua hiyo Tim Irwin kutoka shirika la Umoja Mataifa la kuhudumai watoto UNICEF anasema

(SAUTI TIM)