Hatua za dharura zahitajika kuzuia ukwepaji sheria CAR

Hatua za dharura zahitajika kuzuia ukwepaji sheria CAR

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA, umetoa wito hatua zichukuliwe hima kuzuia ukwepaji sheria na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, siku chache kabla ya uchaguzi wa ubunge na urais nchini humo mnamo Februari 14, 2016. Assumpta Massoi na maelezo kamili.

(Taarifa ya Assumpta)

Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa ujumbe wa MINUSCA, Parfait Onanga-Anyanga, amewasihi wadau wote kuunga mkono mchakato wa uchaguzi, kupinga aina zote za machafuko, na kuheshimu matokeo ya uchaguzi.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa itakayotolewa baadaye mwezi huu inabainisha ukatili na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanywa wakati machafuko yalipozuka Bangui,  mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, kati ya Septemba 26 na Oktoba 20 mwaka 2015.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kipindi hicho kilishuhudia kuwalenga na kuwaua raia, uporaji mkubwa na uteketezaji wa nyumba na mali, miongoni mwa ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu.