Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO iko tayari kusaidia katika harakati dhidi ya Zika: Da Silva

FAO iko tayari kusaidia katika harakati dhidi ya Zika: Da Silva

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo FAO José Graziano da Silva amesema FAO iko tayari kuchangia katika jitihada za kukabiliana na dharura ya kiafya ya virusi vya Zika.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo, Bwana da Silva amesema FAO ina uzoefu wa masuala ya kudhibiti wadudu, na hivyo inaweza kusaidia nchi zilizoathirika katika kubaini hatua za kuchukua bila kuathiri afya ya binadamu au usalama wa chakula na mazingira kupitia matumizi ya kupindukia ya kemikali za kuua wadudu.

Amesema hatua ya msingi ni kuondoa vyanzo vya uzalishaji wa mbu ambavyo ni madimbwi ya maji.

Shirika hilo limetoa mapendekezo kuhusu jinsi ya kutumia kwa ufanisin na usalama viuavijidudu kwa ushirikiano na Shirika la Afya Duniani WHO.