Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haikubaliki kwamba watoto 10,000 wahamiaji huenda wametoweka- UNODC

Haikubaliki kwamba watoto 10,000 wahamiaji huenda wametoweka- UNODC

Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu madawa na uhalifu (UNODC), Yuri Fedotov, amesema leo kwamba, haiwezi kukubalika kuwa huenda watoto wahamiaji 10,000 wasio na wazazi au walezi wametoweka wakiwa safarini kwenda Ulaya,  na kutaka hatua za dharura ichukuliwe kimataifa.

Bwana Fedotov amesema hayo jijini New York, Marekani, wakati wa kikao cha ngazi ya juu kuhusu usafirishaji haramu wa binadamu na kutokomeza utumwa wa kisasa kupitia maendeleo endelevu, ambacho kimeandaliwa na serikali ya Belarus, Kundi la Marafiki Walioungana dhidi ya Usafirishaji Haramu ya Binadamu na UNODC.

Mkuu huyo wa UNODC amesema kuna vymobo vya kutumiwa kupambana na uhalifu huo, ingawa ushirikiano zaidi unahitajika miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na tatizo la usafirishaji haramu wa binadamu.