Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati wa mafuriko Mbeya, Kyela FM ilisaidia wahanga

Wakati wa mafuriko Mbeya, Kyela FM ilisaidia wahanga

Radio, imeendelea kuwa mwokozi wakati wa majanga kwa kuwapatia wananchi taarifa sahihi za jinsi ya kujiokoa. Mathalani nchini Tanzania mwaka 2014 katika mkoa wa Mbeya kusini mwa nchi hiyo, mafuriko yalikumba wakazi wa wilaya ya Kyela na kusababisha uharibifu wa mali. Kituo cha radio ya jamii, Kyela FM kilikuwa mstari wa mbele kuhabarisha umma na hivyo kudhihirisha maudhui ya mwaka huu ya siku ya radio duniani tarehe 13 Februari kuhusu radio wakati wa dharura ikiwemo majanga. Je Kyela FM ilifanya nini? Benson Mwakalinga wa radio hiyo washirika anafafanua katika makala hii.