Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sri Lanka imepiga hatua katika haki za binadamu

Sri Lanka imepiga hatua katika haki za binadamu

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Zeid Ra'ad Al Hussein, amesema Sri Lanka imepiga hatua muhimu katika kuondoa hofu miongoni mwa jamii hususani maeneo ya Colombo na Kusini.

Katika taarifa yake kuhusu hali ya haki za binadamu nchini humo Kamishna Zeid amesema licha ya kwamba maoni yanatofautiana lakini baadhi ya mamabo kama vile utekwaji nyara uliokuwa unasababaisha hofu kwa wanahabari, watetezi wa haki za binadamu, na ambao walikuwa wanathubutu kuikosoa serikali, sasa hufanywa kwa uchache.

Hata hivyo ameonya kuwa licha ya kupungua kwa matukio ya utesaji, bado kuna ripoti ya matukio machache hususani mwaka 2015 ambapo polisi wanadaiwa kutumia nguvu za ziada na kujihusisha na machafuko.

Amepongeza uamuzi wa kuimba wimbo wa taifa kwa lugha za Sinhala na Tamil wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru, ikiwa ni mara ya kwanza tangu miaka ya 1950 akisema hiyo ni ishara ya hatua zilizochukuliwa za kuoboresha mahusino ya jamii.