Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchango wa Redio wakumbukwa Haiti wakati wa tetemeko la ardhi

Mchango wa Redio wakumbukwa Haiti wakati wa tetemeko la ardhi

Mwishoni mwa wiki hii, Umoja wa Mataifa utaadhimisha Siku ya Redio Duniani, mwaka huu siku hiyo ikitumiwa kumulika mchango wa redio wakati wa majanga ya kiasili na mizozo ya kibinadamu.

Katika muktadha huo, tunamulika mchango wa redio wakati wa tetemeko la ardhi, lililotokea nchini Haiti mnamo Januari 12, mwaka 2010.

Majengo ya Umoja wa Mataifa yaliathiriwa na tetemeko hilo la ardhi, na hivyo Redio ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti, MINUSTAH, ikawa imeathiriwa pia, na haikuweza kurejelea kurusha matangazo yake mara moja.

Walter Mulondi ni Msimamizi wa Radio Minustah, na hapa anaeleza umuhimu wa redio ulivyodhihirika kufuatia tetemeko hilo la ardhi la mapema mwaka 2010.

(Sauti ya Walter Mulondi)

Hapa, Bwana Muliondi anaeleza kilichofanyika wakati Radio Minustah FM ilipoanza tena kurusha matangazo yake..

(Sauti ya Walter Mulondi)