Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yazindua shule ya wasichana mjini Qaliqilya

UNRWA yazindua shule ya wasichana mjini Qaliqilya

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina UNRWA kwa kushirikiana na benki ya maendeleo ya Waislamu IDB, wamezindua shule mpya ya wasichana iliyoko mini Qaliqilya mji uliopo katika ukingo wa mto Magharibi.

Uzinduzi wa mpango huo umehudhuriwa na Mkuu wa UNRWA katika ukanda huo Felipe Sanchez, na maafisa kutoka IDB,wanajamii wa Palestina  na wanafunzi.

Akiongea wakati wa hafla hiyo Bwana Sanchez amesema  shule hiyo yenye mazingira bora ni mfano mzuri wa uwekezaji unaoendelezwa na UNRWA katika kuendeleza maendeleo na fursa kwa wakimbizi wa Palestina.

Kwa upande wake mwakilishi wa IDB Abu Diab ameshukuru UNRWA kwa ushirikiano huo unaotoa fursa ya elimu kwa takribani wakimbizi 500,000 wa Palestina.